Hii ni Kwaresma;
Jumatatu asubuhi tarehe 23.03.2026
Mithali 16:7
Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye.
Kwa Yesu kuna upatanisho wa kweli;
Mfalme Suleimani anaonesha ukuu wa Mungu ulioko juu ya mipango ya mwanadamu, akisema kwamba mwanadamu anaweza kupanga lakini hatma yake hutoka kwa Mungu (16:1). Inafundisha umuhimu wa uvumilivu, hatari ya kujisifu, lakini zaidi kumtegemea Bwana. Kwa hiyo msingi wa sura ya 16 ni kumtegemea Bwana katika maisha ya kila siku.
Kwa msingi huo huo wa kumtegemeaBwana, mstari wa 7 tuliousoma unasema njia za mtu zikimpendeza Bwana, hata adui zake huwapatanisha naye. Yaani pamoja na kuwa Kristo ndiye mpatanishi wetu na Mungu, bado anatupatanisha sisi kwa sisi. Kumbe Yesu Kristo ndiye mpatanishi wetu na Mungu, na sisi pia. Tuishi kwa kupatana sisi kwa sisi, kama Yesu alivyotupatanisha na Mungu ili tuufikie mwisho mzuri aliotuahidi. Amina
Uwe na wiki njema yenye upatanisho.
Heri Buberwa Nteboya
Mlutheri
0784 968650
