DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA YA TAREHE 24 MEI, 2026
SIKU YA BWANA YA PENTEKOSTE
NENO LINALOTUONGOZA NI:
“NJOO KWETU ROHO MTAKATIFU”
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Doris Assey.
3. Matoleo ya Tarehe 17/05/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 17/05/2026 ni Washarika 682 na Sunday School 127
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Kesho jumatatu kutakuwa na Ibada ya Pentekoste itakayoanza saa 11 jioni washarika wote mnakaribishwa.
8. Viongozi wa Umoja wa Wanawake wana furaha kuwajulisha washarika kuwa wamevuna asali kutoka kituo chetu cha Tabora. Zitauzwa leo katika ibada zote. Karibuni wote.
9. Shukrani: Vijana walioimba kwaya ya vijana zamani watamtolea Mungu sadaka yao ya shukrani jumapili ijayo 31.05.2026 katika ibada ya tatu Neno: Zaburi 124:1 Wimbo: Kwaya ya vijana wa sasa na Zamani.
Familia ya Mama Perpetua Mamkwe jumapili ijayo 31.05.2026 katika ibada ya tatu watamshukuru Mungu kwa matendo makuu Mungu aliyo watendea. Neno: Zaburi 91:2-7 Wimbo :TMW 391
10. NDOA. Hakuna ndoa za washarika
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Mjini kati: Kwa watashiriki hapa Kanisani saa 1.00 asubuhi
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
- Kinondoni: Kwa Mama Hilda Lwezaula
- Upanga: Kwa Bw & Bi Simbo Nkya
12. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
13. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
