DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI  

MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 14 JUNI, 2026 

SIKU YA BWANA YA 2 BAADA YA UTATU

NENO LINALOTUONGOZA NI:

“YESU NI MLANGO WA KUINGIA MBINGUNI”

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti: 

3. Matoleo ya Tarehe 07/06/2026

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 07/05/2026 ni Washarika 813 na Sunday School 272 

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Leo tarehe 14/06/2026 ni siku ya uchaguzi wa Wazee wa Kanisa katika kila Usharika na Mtaa.

8. Uongozi wa shule ya jumapili unapenda kuwatangazia wazazi kuwa jumamosi ijayo tarehe 20/06/2026 watoto wataanza mazoezi ya nyimbo za tamasha, muda ni saa 8.00 mchana hadi saa 9.00 alasiri. Unaomba ushirikiano wenu Wazazi na Walezi ili watoto wasikose.  

9. NDOA. Ndoa za washarika

 KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 20/06/2026.

 SAA 8.00 MCHANA

  •  Bw. Israel George Mnyitafu na Bi. Rehema Saidi Msangi

 Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.  

10. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Mjini kati: Hapa Usharikani jumamosi saa moja asubuhi

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Kenneth Zebedayo

 

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Peter Mlagha.

- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Bwana na Bibi Itemba

- Oysterbay na Masaki: Kwa Mr & Mrs Desmond Moshi

- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bwana Godfrey Monyo.

- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Kinyaha

 

11. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

 

Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.