Hii ni Kwaresma;
Ijumaa asubuhi tarehe 27.03.2026
Waefeso 1:3-8
3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
4 kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.
6 Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.
7 Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
8 Naye alituzidishia hiyo katika hekima yote na ujuzi;
Kwa Yesu kuna upatanisho wa kweli;
Ni mwanzoni kabisa mwa waraka kwa Waefeso, baada ya Salamu Mtume Paulo anamtukuza Mungu mwenye baraka, aliyewachagua wanadamu na kuweka misingi ya ulimwengu ili wawe watakatifu katika yeye. Paulo anasema Mungu aliwafanya wanadamu kuwa wanawe, sawasawa na mapenzi yake.
Paulo anakazia katika mstari wa saba kwamba kwa damu ya Yesu tunao ukombozi, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake. Hapa Paulo anasema wazi kwamba wanadamu tumepatanishwa na Mungu kwa damu ya Yesu. Mwamini sasa uokolewe. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
Mlutheri
