Hii ni Kwaresma;
Jumamosi asubuhi tarehe 28.03.2026
Ayubu 33:24-30
24 Ndipo amwoneapo rehema, na kusema, Mwokoe asishuke shimoni; Mimi nimeuona ukombozi.
25 Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto; Huzirudia siku za ujana wake;
26 Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia; Hata auone uso wake kwa furaha; Naye humrejezea mtu haki yake.
27 Yeye huimba mbele ya watu, na kusema, Mimi nimefanya dhambi, na kuyapotosha hayo yaliyoelekea, Wala sikulipizwa jambo hilo;
28 Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni, Na uhai wangu utautazama mwanga.
29 Tazama, hayo yote ni Mungu anayeyafanya, Mara mbili, naam, hata mara tatu, kwa mtu,
30 Ili kurudisha roho yake itoke shimoni, Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai.
Kwa Yesu kuna upatanisho wa kweli;
Elihu anaongea na Ayubu, kwamba Mungu siyo mkimya. Anasema Mungu huongea kupitia ndoto, maono, magonjwa, kurejeza mtu toka dhambini na ukombozi wa moja kwa moja. Somo linaonesha Elihu akisema Mungu ni mwenye rehema, mkombozi, hujibu maombi, halipizi ubaya, Mwokozi.
Elihu anamuelezea Mungu kama mwenye rehema, apendaye watu wawe wanyenyekevu kwake na kumcha. Kumbe Imani katika Yesu Kristo ndiyo hutupeleka kwa Mungu mwenye rehema. Yesu tumwaminiye ndiye mpatanishi wetu na Mungu kwa njia ya kifo chake. Tumwamini siku zote za maisha yetu. Amina
Jumamosi njema
Heri Buberwa
