DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA LEO TAREHE 17 MEI, 2026

SIKU YA BWANA KABLA YA PENTEKOSTE

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI:

“MUNGU UTUSIKIE KATIKA KUOMBA KWETU”

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 10/05/2026

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 10/05/2026 ni Washarika 773 na Sunday School 171

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Viongozi wa Umoja wa Wanawake wana furaha kuwajulisha washarika kuwa wamevuna asali kutoka kituo chetu cha Tabora. Zitauzwa jumapili ijayo tarehe 24 Mei 2026 katika ibada zote. Karibuni wote.

8. NDOA. NDOA WASHARIKA

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 23/05/2026 AMBAYO ITAFUNGWA USHARIKA WA KKKT MSASANI KATI YA

  •  Bw. Jerry Edward Ngewe na Bi. Marystella Ernest Swai

 Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Mjini kati: Kwa watashiriki hapa Kanisani saa 1.00 asubuhi

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Eng Elihanan na Mwl Caroline Lema

- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Freeman Mbowe

10. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azaniafront.org, pia tupo Facebook na Instagram.

11. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.