DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 31 MEI, 2026
SIKU YA UTATU MTAKATIFU MUNGU MMOJA: BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI:
“NDUGU WAKAE KWA PAMOJA KWA UMOJA”
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti:
3. Matoleo ya Tarehe 24/05/2026
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 24/05/2026 ni Washarika 570
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
7. Leo tarehe 31/05/2026 tutashiriki chakula cha Bwana. Washarika karibuni.
8. Jumapili ijayo tarehe 07/06/2026 tutamtolea Mungu fungu la Kumi. Washarika tujiandae. Aidha siku hiyo kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa Umoja wa Vijana. Mapendekezo ya majina yamebandikwa kwenye Ubao wa matangzo pamoja na kwenye Mirango ya Kanisa. Kamati ya Malezi mnaombwa kujiandaa kusimamia Uchaguzi huu.
9. NDOA. Ndoa za washarika
KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 20/06/2026.
SAA 8.00 MCHANA
-
Bw. Israel George Mnyitafu na Bi. Rehema Saidi Msangi
Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.
10. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Mjini kati: Kwa watashiriki hapa Kanisani saa 1.00 asubuhi
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Albert Olotu
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Watatangaziana
- Upanga: Kwa Mama Teri. Alykhan Road No. 51
11. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.
-
12. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.
