DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 07 JUNI, 2026

SIKU YA BWANA YA 1 BAADA YA UTATU

NENO LINALOTUONGOZA NI:

“KUMTEGEMEA MUNGU NI MAANDALIZI YA MAISHA YAJAYO”

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 31/05/2026

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 31/05/2026 ni Washarika 873 na Sunday School 263

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Leo tarehe 07/06/2026 tutamtolea Mungu fungu la Kumi. Washarika karibuni

8. Jumanne ijayo tarehe 09/06/2026 saa 11.00 jioni, kutakuwa na mazoezi ya uimbaji kwa ajili ya maandalizi ya mashindano reformation. Kwaya zote mnaombwa kuhudhuria bila kukosa na kufika kwa wakati. Pia washarika mnakaribishwa sana kujiunga na Kwaya kwa maandalizi haya. Mungu awabariki.

9. Uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia wazazi na walezi wenye watoto wa Kipaimara mwaka wa pili kuwa siku ya ijumaa tarehe 12/06/2026 saa 8.30 mchana watoto watafanya mtihani ngazi ya Dayosisi. Hivyo Wazazi na walezi muwahimize wafike kwa wakati asikosekane mtoto hata mmoja.

10. Jumapili ijayo tarehe 14/06/2026 ni siku ya uchaguzi wa Wazee wa Kanisa katika kila Usharika na Mtaa. Washarika tuiombee siku hiyo.

11. NDOA. Ndoa za washarika

 KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 20/06/2026.

 SAA 8.00 MCHANA

  •  Bw. Israel George Mnyitafu na Bi. Rehema Saidi Msangi

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Mjini kati: Kwa Lyinda Felician Mtaa wa Nkuruma

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mwemezi Mutembei.

13. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

14. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.