Date: 
11-06-2026
Reading: 
Kumbukumbu la Torati 6:16-19

Alhamisi asubuhi tarehe 11.06.2026

Kumbukumbu la Torati 6:16-19

16 Msimjaribu Bwana, Mungu wenu, kama mlivyomjaribu huko Masa.

17 Zishikeni kwa bidii sheria za Bwana, Mungu wenu, na mashuhudizo yake, na amri zake alizokuagiza.

18 Nawe fanya yaliyo sawa, na mema, machoni pa Bwana; ili mpate kufanikiwa, nawe upate kuingia na kuimiliki nchi nzuri Bwana aliyowaapia baba zako,

19 ya kuwa atawasukumia nje adui zako wote mbele yako, kama alivyosema Bwana.

Kumtegemea Mungu ni maandalizi ya maisha yajayo;

Asubuhi ya leo tunasoma Israeli wakipewa tahadhari ya kutotii. Wanaelekezwa kumkumbuka na kumtii Bwana aliyewatoa utumwami Misri. Mistari kabla ya somo inasomeka;

Kumbukumbu la Torati 6:12-14

12 ndipo ujitunze, usije ukamsahau Bwana aliyekutoa nchi ya Misri, nyumba ya utumwa.
13 Mche Bwana, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake.
14 Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao;

Somo linaendelea kuwaambia Israeli kutomjaribu Bwana Mungu wao, kuzishika sheria, lakini kufanya yaliyo mema machoni pa Bwana ili kufanikiwa na kuingia nchi ya ahadi. Kwa hiyo Israeli wanaelekezwa kutomuacha Bwana. Nasi tusimuache Bwana, ili akirudi asituache. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa