Date: 
02-03-2026
Reading: 
Matendo ya mitume 3:1-5

Hii ni Kwaresma 

Jumatatu asubuhi tarehe 02.03.2026

Matendo ya Mitume 3:1-5

1 Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa.

2 Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu.

3 Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka.

4 Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi.

5 Akawaangalia, akitaraji kupata kitu kwao.

Ukatili upo, tuupinge;

Tunamsoma kiwete mmoja ambaye kwa maisha yake yote alikuwa anakaa hekaluni mlangoni ili aombe kupata chochote kutoka kwa watu waliokuwa wakiingia hekaluni. Aliomba kwa wote, na hata alipowaona Petro na Yohana aliomba kupata kitu kwao. Somo linaonesha kuwa alitarajia kupata kitu kwao. Petro na Yohana hawakumpa kwa jinsi alivyotarajia, bali kumuombea uponyaji kama tunavyosoma;

Matendo ya Mitume 3:6-8

6 Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.
7 Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu.
8 Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu Mungu.

Somo linasema kiwete alitegemea kupata "sadaka" lakini akapata zaidi ya hiyo sadaka, akapona, akatembea nao kuingia hekaluni. Alirukaruka, akimsifu Mungu. Petro alimuombea uponyaji kiwete kwa jina la Yesu. Kumbe wokovu wetu ni kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye anatuita kuupinga ukatili. Amina

Uwe na wiki njema isiyo na ukatili

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650