Date: 
05-03-2026
Reading: 
Kutoka 14:5-10

Hii ni Kwaresma;

Alhamisi asubuhi tarehe 05.03.2026

Kutoka 14:5-10

5 Mfalme wa Misri aliambiwa ya kuwa wale watu wamekwisha kimbia; na moyo wa Farao, na mioyo ya watumishi wake, iligeuzwa iwe kinyume cha hao watu, nao wakasema, Ni nini jambo hili tulilotenda, kwa kuwaacha Waisraeli waende zao wasitutumikie tena?

6 Akaandalia gari lake, akawachukua watu wake pamoja naye;

7 tena akatwaa magari mia sita yaliyochaguliwa, na magari yote ya Wamisri, na maakida juu ya magari hayo yote.

8 Na Bwana akaufanya moyo wake Farao mfalme wa Misri kuwa mgumu, naye akawafuata wana wa Israeli; kwa sababu wana wa Israeli walitoka kwa ujeuri.

9 Wamisri wakafuata nyuma yao, farasi zote na magari yote ya Farao, na askari zake wenye kupanda farasi, na jeshi lake, nao wakawapata hali wamepanga pale karibu na bahari, karibu na Pi-hahirothi, kukabili Baal-sefoni.

10 Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua macho yao, na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia Bwana.

Ukatili upo, tuupinge;

Haikuwa rahisi kwa Israeli kuondoka Misri, maana Farao hakuwa tayari kuwaruhusu waondoke. Ni baada ya mapigo kumi, pigo la mwisho likiwa kifo cha mzaliwa wa kwanza kwa kila familia, ndipo Farao aliwaruhusu kuondoka. Baada ya hapo walipewa maelekezo kuhusu Pasaka, siku ya mikate isiyotiwa chachu na maelekezo mengine, wakaondoka.

Somo ndipo linakuja, Israeli wanaelekea bahari nyekundu. Farao akaendelea kuwa na moyo mgumu, akajuta kuwaruhusu Israeli waondoke! Akaamuru wafuatwe! Lakini Farao na jeshi lake waliishia kufa baharini. Jeshi la Farao liliangamia baharini kwa sababu ya Farao kuwa na moyo mgumu. Farao alikuwa katili. Ukatili hauna faida yoyote zaidi ya dhambi na hasara. Tuache ukatili. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa