Date: 
20-03-2026
Reading: 
Yohana 6:26-29

Hii ni Kwaresma 

Ijumaa asubuhi tarehe 20.03.2026

Yohana 6:26-29

[26]Yesu akawajibu, akasema, Amin, amin, nawaambieni, Ninyi mnanitafuta, si kwa sababu mliona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba.

[27]Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.

[28]Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu?

[29]Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye.

Yesu ni chakula cha uzima;

Yesu anawaambia waliomfuata baada ya kushiba mikate na samaki kuwa wanamfuata kwa sababu ya mikate, na siyo kwa sababu ya ishara! Anawaambia wasikitendee kazi chakula kiharibikacho, bali kidumucho hata uzima wa milele. Yaani wamwamini Yesu, aliye chakula cha uzima.

Wito huu unatujia asubuhi ya leo, kuwa tusimfuate Yesu kwa ajili tu ya tamaa zetu, bali tumwamini na tumfuate kwa utii wa neno lake, yeye aliye chakula kisichoharibika, kwa uzima wa milele.

Ijumaa njema.

 

Heri Buberwa