Date: 
21-03-2026
Reading: 
Yohana 17:1-3

Hii ni Kwaresma 

Jumamosi asubuhi tarehe 21.03.2026

Yohana 17:1-3

1 Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe;

2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.

3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Yesu ni chakula cha uzima;

Inaaminika kwamba sura ya 17 ya Injili ya Yohana ndiyo sala ndefu aliyosali Yesu, iliyoandikwa. Alikuwa anawaombea wanafunzi wake. Katika sala hiyo (mst 2 na wa 3) anawaombea wote Baba aliompa awape uzima wa milele ambao ni kumjua Mungu wa kweli kwa njia ya Yesu Kristo mwanae.

Yesu alipowaombea wanafunzi wake kumjua yeye, aliwaombea umoja pia ili wakae kwa pamoja na kuifanya kazi yake. Naweza kusema kuwa Yesu alikuwa analiombea Kanisa lake, ili wote tumjue yeye. Basi na tumjue yeye aliye chakula cha uzima, ili atuokoe na kutupa uzima wa milele. Amina

Jumamosi njema

Heri Buberwa