Date: 
30-03-2026
Reading: 
2 Wafalme 9:13

Hii ni Kwaresma;

Jumatatu asubuhi tarehe 30.01.2026

2 Wafalme 9:13

Basi wakafanya haraka, kila mtu akalitwaa vazi lake, na kulitia chini yake juu ya madaraja, wakapiga baragumu wakasema, Yehu ni mfalme.

Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana;

Nabii Elisha alimtuma Nabii mmojawapo (hatajwi jina) aende huko Gileadi, akamtafute Yehu mwana wa Yehoshafati, amuondoe katika nyumba ya ndugu zake amtie mafuta na kuwa Mfalme wa Israeli. Nabii huyo alimkuta Yehu akiwa na majemadari wenzake akampaka mafuta na kumtangazia Ufalme. Mstari tuliousoma ni hatua ya mwisho kwa Yehu Mfalme, ambapo watumishi wa bwana wake (Yehu) wanaweka mazingira vizuri na kupiga baragumu kutangaza kwamba Yehu ni mfalme.

Tulichokisoma ulikuwa ni utaratibu wa kupata Mfalme. Wafalme hawa walitawala kwa mamlaka yote. Ilipobidi waliua ili kuweka mambo sawa katika ufalme wao. Wafalme walitawala, manabii walileta ujumbe wa Mungu, makuhani walihudumu hekaluni. Hivi ndivyo watu waliongozwa. Lakini Kristo alipofanyika mwana-kondoo wa pasaka aliuondoa ufalme na ukuhani wa namna hiyo. Hakuna ufalme wa kibabe wala ukuhani wa mbuzi na damu. Yesu Kristo anatosha. Amina

Uwe na wiki njema

 

Heri Buberwa