Date: 
16-04-2026
Reading: 
Yohana 21:18-23

Hii ni Pasaka;

Alhamisi asubuhi 16.04.2026

Yohana 21:18-23

18 Akasema, Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka.

19 Akasema neno hilo kwa kuonyesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, Nifuate.

20 Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?)

21 Basi Petro akamwona huyo, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je?

22 Yesu akamwambia, Ikiwa nataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje wewe? Wewe unifuate mimi.

23 Basi neno hilo lilienea katikati ya ndugu ya kwamba mwanafunzi yule hafi. Walakini Yesu hakumwambia ya kwamba hafi; bali, Ikiwa nataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje wewe?

Yesu Kristo ajidhihirisha kwa wanafunzi wake;

Yesu baada ya kufufuka aliwatokea wanafunzi wake kabla ya kupaa. Wakati anawatokea mara ya tatu ilikuwa kwenye bahari ya Tiberia, ambapo aliwawezesha kupata samaki maana walikuwa wamekesha bila kupata kitu. Petro na wenzake walikuwa wamerudia kazi yao maana hawakuona uelekeo. Yesu akawapa mkate na samaki, wakala.

Yesu alimuita Petro mara tatu, akimpa utume wa kulisha kondoo zake.

Somo la asubuhi hii linaanza kwa kuonesha mkazo wa Yesu kwa Petro akimtuma kuitenda kazi yake pasipo ulegevu. Petro anamuuliza Yesu kuhusu mwanafunzi aliyempenda (Yohana Mtume), lakini Yesu anamkazia Petro kumtumikia Bwana. Yesu anajidhihirisha kwetu akituita kumwamini na kumtumikia. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa