Date: 
07-05-2026
Reading: 
Zaburi 30:1-4

Hii ni Pasaka;

Alhamisi asubuhi tarehe 07.05.2026

Zaburi 30:1-4

1 Ee Bwana, nitakutukuza kwa maana umeniinua, Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu.

2 Ee Bwana, Mungu wangu, Nalikulilia ukaniponya.

3 Umeniinua nafsi yangu, Ee Bwana, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao shimoni.

4 Mwimbieni Bwana zaburi, Enyi watauwa wake. Na kufanya shukrani. Kwa kumbukumbu la utakatifu wake.

Njooni tumsifu Mungu wetu;

Mfalme Daudi anaimba akimtukuza Mungu kwa kumuinua, anasema Mungu hakuwafurahisha adui zake juu yake (Daudi). Daudi anaendelea kusema alimlilia Bwana akamponya, na kumtoa mikononi mwa wabaya. Anawaita watu kumwimbia Bwana Zaburi, walio watauwa wake.

Kama Daudi anavyokiri kuinuliwa na Bwana, sisi nasi tumeinuliwa na Bwana kwa kutuokoa, lakini kwa jinsi anavyotutunza katika maisha ya kila siku. Hivyo tunawajibika kumsifu Mungu kwa kutuinua na kutufanya watu wake. Tumsifu yeye daima kwa kuwaza, kunena na kutenda kwa kadri ya mapenzi yake. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa