Date: 
09-05-2026
Reading: 
Matendo ya Mitume 16:25-30

Hii ni Pasaka;

Jumamosi asubuhi tarehe 09.05.2026;

Matendo ya Mitume 16:25-30

25 Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.

26 Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.

27 Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia.

28 Ila Paulo akapaza sauti yake kwa nguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa.

29 Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa hofu, akawaangukia Paulo na Sila;

30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?

Njooni tumsifu Mungu wetu;

Paulo na Sila walikuwa wamefungwa gerezani, usiku wa manane wakamfanyia Mungu ibada kwa kuimba nyimbo za kumsifu, wafungwa wengine wakiwasikiliza. Ghafla tetemeko la nchi likasababisha milango ya gereza kufunguka, Paulo na Sila wakatoka gerezani. Mlinzi wa gereza aliogopa akataka kujidhuru, Paulo akamzuia. Yule mlinzi aliamini akabatizwa na familia yake usiku uleule.

Ibada ya kumsifu Mungu ilisababisha Paulo na Sila kutolewa gerezani. Mungu aliipokea ibada yao ya sifa. Ni ujumbe unaotutaka kumfanyia Bwana ibada tukimsifu kwa sababu ya ukuu wake. Ibada njema hutaja sifa za Mungu. Tuhakikishe tunampa sifa Mungu pekee, tukimsifu bila kuchoka. Sifa kuu ni kutenda yaliyo mema. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa