Date: 
11-05-2026
Reading: 
Yeremia 29:11-12

Hii ni Pasaka;

Jumatatu asubuhi tarehe 11.05.2026;

Yeremia 29:11-12

11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

12 Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.

Imetupasa kumwomba Mungu siku zote;

Ujumbe tunaousoma asubuhi ya leo ni ahadi ya Mungu kwa wana wa Israeli waliokuwa uhamishoni, akiwahakikishia kwamba pamoja na magumu waliyokuwa wanapitia, bado alikuwa na mpango nao wa kuwarejesha, kuwapa amani na tumaini. Ahadi ilikuwa kwa ajili ya Wayahudi waliokuwa Babeli waliokuwa uhamishoni kwa miaka 70. Haikuwa ahadi ya kutoka upesi Babeli, lakini yenye tumaini katikati ya wakati mgumu.

Kwa kurejea historia, somo tulilosoma ulikuwa ni ujumbe kwa Israeli. Kwa leo naweza kusema ujumbe huu unatukumbusha kuwa Mungu wetu habadiliki, hutuhudumia katika nyakati zote hata zile ngumu akitimiza ahadi zake kwa waaminio. Kwa hiyo tuwe nayo hakika kuwa Mungu yuko nasi daima, tusitetereke. Amina

Uwe na wiki njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

Mlutheri 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com