DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI

MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 10 MEI, 2026

SIKU YA BWANA YA 5 BAADA YA PASAKA

NENO LINALOTUONGOZA NI:

“IMETUPASA KUMWOMBA MUNGU SIKU ZOTE”

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Matoleo ya Tarehe 03/05/2026

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

- 0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada za tarehe 03/05/2026 ni Washarika 727

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Ibada ya asubuhi saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada ya mchana saa 7.00 mchana. Ijumaa saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.

7. Alhamisi ijayo tarehe 14/05/2026 kutakuwa na ibada ya kupaa kwa Yesu Kristo. Kwaya zote zitahudumu. Zamu za wazee itakuwa ni kundi la Kwanza.

8. Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) mkoa wa Dar es Salaam idara ya Wanawake wameandaa Kongamano la maombi litakalofanyika Usharika wa Moravian Tabata Liwiti tarehe 16 Mei, 2026 kuanzia saa 2.00 asubuhi mpaka saa 7.00 mchana. Kongamano hili litaongozwa na Baba Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa. Siku hiyo vazi rasmi itakuwa ni kitenge cha CCT ambacho kinapatikana duka la KKKT posta Tancot house na WAMA Buguruni kwa bei ya sh. 33,000/=.

9. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 17/05/2026 katika ibada ya Tatu saa 4.30 asubuhi

- Familia ya Hayati Mzee Cleopa David Msuya watamshukuru Mungu kwa faraja na Baraka nyingi alizowajalia tangu kutwaliwa kwa Mzee Cleopa David Msuya mwaka mmoja uliopita tarehe 07 Mei, 2025 na miaka 21 tangu kutwaliwa kwa mpendwa wao Geofrey Cleopa Msuya tarehe 15 Mei, 2005 pamoja na matendo mengi aliyowatendea.

Neno: Thesolanike 4:14, Wimbo: TMW 159

10. NDOA. NDOA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 23/05/2026 AMBAYO ITAFUNGWA USHARIKA WA KKKT MSASANI KATI YA

  •  Bw. Jerry Edward Ngewe na Bi. Marystella Ernest Swai

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

11. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

- Mjini kati: Kwa watashiriki hapa Kanisani saa 1.00 asubuhi

- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Mkwe

- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Nyamajeje Buchanagandi

- Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Mama Upendo Mkandawile

- Oysterbay na Masaki: Kwa Anord Charles Mkony

- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Watashiriki ibada ya kupaa alhamisi hapa usharikani.

- Upanga: Watashiriki ibada ya maombi ijumaa hapa usharikani

12. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front. org, pia tupo Facebook na Instagram.

13. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.