Date:
15-05-2026
Reading:
Matendo ya Mitume 1:9-11
Ijumaa asubuhi tarehe 15.05.2026
Matendo ya Mitume 1:9-11
[9]Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.
[10]Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe,
[11]wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.
Yesu achukuliwa juu mbinguni;
Baada ya Yesu kufufuka, alipaa mbinguni baada ya siku 40, akirudi kwa Baba yake. Ni baada ya kazi yake hapa duniani, kama Mungu kweli na mwanadamu kweli.
Kupaa kwa Yesu kuliashiria nini?
1. Kupaa kwa Yesu kuliashiria kazi yake hapa duniani kumalizika.
2. Kupaa kwa Yesu kuliashiria kuendelea kwa kazi yake, akiwa mbinguni.
3. Kupaa kwa Yesu kuliashiria mwanzo wa sisi kufanya utume wake kama alivyotutuma.
Kama tulivyoona,Yesu alipaa kwenda mbinguni baada ya siku 40, na bado anaendelea kutenda kazi yake kwa wote wamwaminio. Tuendelee kumwamini huyu Yesu aliyepaa, maana alikuwepo, yupo na ataendelea kuwepo, na mwisho atarudi kulichukua Kanisa lake. Amina
Siku njema.
Heri Buberwa
