Date: 
16-05-2026
Reading: 
Luka 24:50-53

Jumamosi asubuhi tarehe 16.05.2026;

Luka 24:50-53

50 Akawaongoza mpaka Bethania, akainua mikono yake akawabariki.

51 Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni.

52 Wakamwabudu; kisha wakarudi Yerusalemu wenye furaha kuu.

53 Nao walikuwa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu.

Yesu achukuliwa juu mbinguni;

Neno la asubuhi hii ni mwisho wa Injili ya Luka akiandika jinsi Yesu alivyopaa. Baada ya kufufuka na kuwatokea wanafunzi, Luka anaonesha Yesu akiwabariki wanafunzi wake kisha kujitenga nao na kuchukuliwa mbinguni. Yesu alikuwa amehitimisha kazi yake hapa duniani, tukio la kupaa likishuhudiwa na wanafunzi wake.

Luka anaandika kwamba wanafunzi walirudi Yerusalemu kwa furaha kuu, wakakaa daima hekaluni wakimsifu Mungu. Kukaa hekaluni wakimsifu Mungu ni ishara ya wanafunzi kudumu katika imani na kudumu katika utume walioachiwa na Yesu Kristo. Nasi tudumu katika imani, tukitenda yatupasayo kama tulivyoitwa. Amina

Jumamosi njema

 

Heri Buberwa 

Mlutheri