Date: 
19-05-2026
Reading: 
Mwanzo 25:21-22

Jumanne asubuhi tarehe 19.05.2026

Mwanzo 25:21-22

21 Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.

22 Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana.

Mungu utusikie katika kuomba kwetu;

Asubuhi ya leo tunamsoma Isaka akimuomba Mungu kwa ajili ya mke wake (Rebeka) aliyekuwa tasa, Bwana akasikia sala yake na Rebeka akabeba mimba ya mapacha. Alijifungua hao watoto wawili mapacha, wakati huo Isaka akiwa na umri wa miaka sitini.

Ujumbe wa asubuhi ya leo umo katika tendo la Isaka kumuomba Bwana kwa ajili ya mke wake aliyekuwa tasa akapata mapacha. Bwana alisikia kuomba kwake. Hata sisi leo tunakumbushwa kuomba kwa imani, maana Bwana husikia kuomba kwetu. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa