Date: 
22-05-2026
Reading: 
Maombolezo 3:52-57

Ijumaa asubuhi tarehe 22.05.2026

Maombolezo 3:52-57

52 Walio adui zangu bila sababu Wameniwinda sana kama ndege;

53 Wameukatilia mbali uhai wangu gerezani, Na kutupa jiwe juu yangu.

54 Maji mengi yalipita juu ya kichwa changu, Nikasema, Nimekatiliwa mbali.

55 Naliliitia jina lako, Bwana, kutoka lile shimo Liendalo chini kabisa.

56 Ukaisikia sauti yangu; usifiche sikio lako Ili usisikie pumzi yangu, kwa kilio changu.

57 Ulinikaribia siku ile nilipokulilia; Ukasema, Usiogope.

Mungu utusikie katika kuomba kwetu;

Mwandishi anawaalika watu kutafakari maisha yao, kutubu na kumrudia Bwana. Mstari wa 55 ni wito wa kuliitia jina la Bwana, halafu mstari wa 56 unatoa hakika ya Bwana kuisikia sauti ya wamuitao na kujibu kilio chao. Mungu anaonekana kuwa karibu na watu wake akiwaambia "usiogope".

Sura ya 3 ya kitabu cha Maombolezo inakataza imani ya maigizo, na kuelekeza imani ya kweli, upendo na toba ya kweli. Katika yote hayo, mistari tuliyoisoma inatupa ujumbe wa kumuita Bwana, kwa ahadi ya kutusikia tukiambiwa "usiogope". Mungu awe kiongozi wetu, tukidumu katika kumuomba kwa imani maana yeye hujibu maombi yetu. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa