Date: 
23-05-2026
Reading: 
Yakobo 1:5-11

Jumamosi asubuhi tarehe 23.06.2026

Yakobo 1:5-11

5 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.

7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.

8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.

9 Lakini ndugu asiye na cheo na afurahi kwa kuwa ametukuzwa;

10 bali tajiri kwa kuwa ameshushwa; kwa maana kama ua la majani atatoweka.

11 Maana jua huchomoza kwa hari, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.

Mungu utusikie katika kuomba kwetu;

Yakobo anafundisha juu ya hekima na imani. Anasema mtu akipungukiwa na hekima, aombe kwa Mungu, kwa imani pasipo shaka yoyote. Yakobo anaendelea kusema kwamba mtu wa nia mbili husitasita katika njia zake zote, hivyo anasisitiza kuomba kwa imani, kwa Mungu bila woga. 

Ujumbe wa Yakobo ni kuishi maisha ya kuomba, tena kuomba kwa imani. Kwa hiyo asubuhi ya leo tunakumbushwa kuomba kwa imani, kwenye jambo lolote. Kuomba yawe maisha yetu, tukizingatia kuomba tukitimiza wajibu katika kazi zetu. Yaani omba, tafuta, bisha, Mungu anasikia kuomba kwako. Amina

Siku njema

 

Heri Buberwa