Date:
30-05-2026
Reading:
Waebrania 2:1-4
Hii ni Pentekoste;
Jumamosi asubuhi 30.05.2026;
Waebrania 2:1-4
1 Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa.
2 Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,
3 sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;
4 Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.
Roho Mtakatifu ni nguvu yetu;
Somo la asubuhi ya leo ni onyo la kuwa makini katika njia ya wokovu. Mwandishi wa waraka kwa Waebrania anakazia kuamini Injili iliyohubiriwa. Anasema hakuna kupona pasipo kujali wokovu mkuu namna hii, yaani wokovu ulioletwa na Yesu Kristo.
Mwandishi anasema wokovu ulinenwa na Bwana, ukathibitika kwa waaminio. Mungu akazidi kuwatokea watu wake kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, sasa kwa njia ya Roho Mtakatifu. Wito wa leo ni kusimama katika Kristo aliye njia ya kweli na uzima. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
