Date:
12-06-2026
Reading:
Zaburi 37:3-6
Ijumaa asubuhi tarehe 12.06.2026
Zaburi 37:3-6
3 Umtumaini Bwana ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.
4 Nawe utajifurahisha kwa Bwana, Naye atakupa haja za moyo wako.
5 Umkabidhi Bwana njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.
6 Ataitokeza haki yako kama nuru, Na hukumu yako kama adhuhuri.
Kumtegemea Mungu ni maandalizi ya maisha yajayo;
Daudi anaimba juu ya uvumilivu katika maisha ya imani. Katika uvumilivu huo anasema inafaa kumtumaini Bwana na kutenda mema, na kuwa mwaminifu. Daudi anasema upo uhakika wa haja za mioyo ya waaminio toka kwa Bwana. Anakazia kumkabidhi Bwana njia na kumtumaini maana atafanya.
Daudi anaonesha ahadi ya Mungu kwa wale wamwaminio. Tukiwa wavumilivu katika maisha yetu ya imani Bwana anatufurahisha na kutupa haja za mioyo yetu. Tumkabidhi Bwana njia zetu, naye atafanya. Huko ndiko kumtegemea Mungu kwa ajili ya maisha yajayo. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
