Date:
16-06-2026
Reading:
Yeremia 13:15-17
Jumanne asubuhi 16.06.2026
Yeremia 13:15-17
15 Sikilizeni ninyi, kategeni masikio yenu; msifanye kiburi; maana Bwana amenena.
16 Mtukuzeni Bwana, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene.
17 Bali kama hamtaki kusikia, roho yangu italia kwa siri, kwa sababu ya kiburi chenu; na jicho langu litalia sana na kutoka machozi mengi, kwa kuwa kundi la Bwana limechukuliwa hali ya kufungwa.
Yesu ni mlango wa kuingia mbinguni;
Somo la leo asubuhi ni sehemu ya ujumbe wa Yeremia kwa Israeli, uliokuwa na tishio la kupelekwa uhamishoni. Israeli walikuwa wanaambiwa kutega sikio pasipo kiburi wakimsikiliza Bwana, ambaye alikuwa ananena nao kuhusu utii kwake. Wanaambiwa kumtukuza Bwana kabla hajaleta giza.
Katika mstari wa 17 wanapewa onyo, kwamba kama hawawezi kumsikia Bwana kwa sababu ya kiburi chao watakuwa mateka. Ulikuwa ni ujumbe wa onyo kama tulivyoona, na Israeli walipelekwa uhamishoni vilevile. Tumsikilize Kristo na kumtii ili tuingie mbinguni, maana yeye ndiye mlango wa kuingia huko mbinguni. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
