Date:
19-06-2026
Reading:
Amosi 5:14-15
Ijumaa asubuhi tarehe 19.06.2026;
Amosi 5:14-15
14 Tafuteni mema, wala si mabaya, mpate kuishi; hivyo Bwana, Mungu wa majeshi, atakuwa pamoja nanyi, kama msemavyo.
15 Yachukieni mabaya; yapendeni mema; mkaithibitishe haki langoni; yamkini kwamba Bwana, Mungu wa majeshi, atawafanyia fadhili mabaki ya Yusufu.
Yesu ni mlango wa kuingia mbinguni;
Amosi anakemea uovu katika sura ya nne, haki iliyopotea, ibada za sanamu, kutojali, unafiki wa kiimani na kutomcha Bwana. Mistari tuliyosoma inaelekeza watu kuacha uovu, ujumbe ukiwa ni kutafuta yaliyo mema ili wapate kuishi. Amosi anawataka kuyachukia mabaya na kupenda mema, huo ukiwa wito wa kumrudia Bwana.
Uovu lazima ukemewe, uachwe na kundi la waaminio. Kuuacha uovu ni vigumu pasipo msaada wa Roho Mtakatifu, Mungu mwenyewe. Tuyachukie mabaya, tupende mema, na wema wa Bwana utakuwa pamoja nasi. Yesu Kristo anatuita kuacha uovu na kutenda mema. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
Mlutheri
